Barua ya Ruge Mutahaba kwa Vijana wa kitaa.

 Barua ya Ruge Mutahaba kwa Vijana wa kitaa.



Ni muda sasa sijaongea na wewe kijana, tangu safari yangu kuisha. Amini kuwa bidii  huleta ubora, usimwache bidii aende zake. Kwahiyo kijana usikate tamaa, tena kataa kushika tama.


Ni muda sasa sijaongea na wewe kijana haimanishi nimekusahau ni ugeni tu wa huku nilipo kuja. Kwa kuwa mambo yalikuwa mengi nilihitaji kujipanga kidogo.


Lakini nakukumbuka,bado unaishi kwenye moyo wangu. Kila mara nikikumbuka mapambano yetu tuliyokuwa tukifanya tukiwa pamoja, ya kujenga Tanzania tunayoitaka. Huwa na tabasamu linanijia, usiulize kwanini? Kwa sababu hii ndio Tanzania ninayoitamani. Bila shaka utanisaidia kutimiza ndoto yangu.


Nikukumbushe tu kijana, amani ndio tunu inayofunika juhudi na uchapakazi. Ambayo ndio sifa kuu ya Tanzania.


Kama niliyokuambia kijana, tulivyo kuwa wote ndoto si ile unayoota ukiwa usingizini, ndoto ni ile inayokufanya usipate usingizi.


Amka! Amka! Dunia inakusubiri, sioni haja ya kukupigia yowe la kukupongeza. Hongera! Hongera! Kwa kuwa na ndoto kubwa mana binafsi sijawahi kuwa na ndoto ndogo.


Ni bora uwaze kuwa jua, ukishindwa uwe nyota. Kwa hakika najua unapitia wakati mgumu, mara zote kumbuka hakuna ushindi unaokuja bila maumivu na jasho. Pambana! Usikate tamaa.


Ni muda sasa sijaongea na wewe kijana, tangu safari yangu kuisha. Amini kuwa bidii  huleta ubora, usimwache bidii aende zako.Kwahiyo kijana usikate tamaa, tena kataa kushika tama.


Woow! Woow! Binti aliyekuwa nyuma ya pazia wakati wote, namuona mstali wa mbele akiongoza mapambano, sambamba kabisa na wapambanaji wengine.


Hakuna unyonge tena, unanikumbusha ule usemi wa kuwa ‘matikiti na matango huponya njaa japokuwa hayawekwi kwenye kundi la vyakula.’ 


Tanzania itajengwa na watanzania wote wenye nia, ama kwa hakika jua litachomoza kesho tena.


Kijana kumbuka teknolojia, ubunifu iendelee kuwa silaha ya kubadilisha maisha yako, mabadiliko ya fikra, mtazamo wako, na misimamo yako.


Usisubiri wengine wafanye, eti ndio ufanye! Ukiamua kufanya, usifanye tuu, fanya sana.

Kasi yenye manufaa ni ile itakayokufikisha kule unapopataka kwenda. Kwa kuwa kwenda sio kunyanyua miguu tu. bali hata mwendaazimu ananyanyua mguu kwenda lakini jioni, amerudi amevaa makorokoro kichwani.


Amini kuwa bidii huleta ubora, usimuache bidii aende zake.


Ahsante kijana, ahsante kwa kukubali kubeba jukumu la kubeba Tanzania bora kuliko uliyoikuta. Asante kwa kupokea barua yangu hii kijana.


Wewe ni kijana wa kitaa, nakutia moyo, kaza mwendo, songa mbele!  


You Might Also Like

0 #type=(blogger)

Top Categories