Mbali na Nyumbani - Adam Shafi

Mbali na Nyumbani  ni riwaya ya kitawasifu inayosimulia ari ya mhusika mkuu ya kukisaka kipendacho roho. Ukosapo mapenzi utaondoka nyumbani uende mbali ukayasake; ukosapo masomo utafanya vivyo hivyo. Ukosapo marafiki au kazi utajipata barabarani ukitamba na njia kwenda kuisaka. Je, unaposukumwa na ari au utundu huo na kuizima kiu ya kujua usiyoyajua? Kama ni kutafuta maarifa, hiyo ni heri…mpaka safari igeukapo kuwa na shari ndipo utakapobaini ukweli kwamba nyumbani hamna mfanowe hata pawe ni pangoni.   Adam Shafi katika maisha ya kiuhalisia anatoka nyumbani kwao Zanzibar akiwa amefumwa na mkuki wa kiu ya elimu. Anapofika Bungoma anaselelea. Anafanya yote ya kufanywa na kijana wa rika lake. Kisha anatumia ujanja wake kuvuka mpaka na akajipata nchini uganda. Anapofika Khartoum karibu tamaa ya kuendelea na safari inamwondokea. Kula ni kwa nadra na kulala ni taabutupu. Hatimaye anajipata Kairo. Anaporudi Zanzibar, nyumbani hapamweki. Mara hii anajipata Ujerumani kwa ufadhili wa kisiasa, ambako pia panamkataa. Kisa na maana?   Mbali na nyumbani ni kisa cha matukio halisi lakini chenye msuko wa kiriwaya na chenye sifa zote za riwaya.   Adam Shafi ni mwandishi mwenye tajriba katika utunzi wa riwaya za kiswahili. Anayoyasema yamempitikia, ameyashuhudia, ameyahisi na yamemfika, ama katika ndoto au katika hali halisi.


 Mbali na Nyumbani  ni riwaya ya kitawasifu inayosimulia ari ya mhusika mkuu ya kukisaka kipendacho roho. Ukosapo mapenzi utaondoka nyumbani uende mbali ukayasake; ukosapo masomo utafanya vivyo hivyo. Ukosapo marafiki au kazi utajipata barabarani ukitamba na njia kwenda kuisaka. Je, unaposukumwa na ari au utundu huo na kuizima kiu ya kujua usiyoyajua? Kama ni kutafuta maarifa, hiyo ni heri…mpaka safari igeukapo kuwa na shari ndipo utakapobaini ukweli kwamba nyumbani hamna mfanowe hata pawe ni pangoni.


Adam Shafi katika maisha ya kiuhalisia anatoka nyumbani kwao Zanzibar akiwa amefumwa na mkuki wa kiu ya elimu. Anapofika Bungoma anaselelea. Anafanya yote ya kufanywa na kijana wa rika lake. Kisha anatumia ujanja wake kuvuka mpaka na akajipata nchini uganda. Anapofika Khartoum karibu tamaa ya kuendelea na safari inamwondokea. Kula ni kwa nadra na kulala ni taabutupu. Hatimaye anajipata Kairo. Anaporudi Zanzibar, nyumbani hapamweki. Mara hii anajipata Ujerumani kwa ufadhili wa kisiasa, ambako pia panamkataa. Kisa na maana?


Mbali na nyumbani ni kisa cha matukio halisi lakini chenye msuko wa kiriwaya na chenye sifa zote za riwaya.


Adam Shafi ni mwandishi mwenye tajriba katika utunzi wa riwaya za kiswahili. Anayoyasema yamempitikia, ameyashuhudia, ameyahisi na yamemfika, ama katika ndoto au katika hali halisi. 


Kuhusu Mwandishi

Adam Shafi alizaliwa mjini Zanzibar mwaka 1940, baada ya elimu yake ya shule ya msingi alijiunga na chuo cha ualimu cha Seyyia Khalifa ( sasa chuo cha ualimu cha Nkurumah) mwaka 1957 hadi mwaka 1960.


Alipata diploma ya juu katika fani ya siasa ya uchumi katika fani ya siasa ya uchumi katika chuo cha Fritz Heckert, katika iliyokuwa jamhuri ya kidemokrasia ya ujerumani mwaka 1963.


Alipata mafunzo ya uandishi wa habari mjini Prague, nchini Czechoslovakia (sasa jamhuri ya Czesh), mwaka 1964 hadi mwaka 1965, nchini Sweden mwaka 1982 na nchini Marekani mwaka 1985.


Adam Shafi alikuwa mwenyeketi wa Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA) kuanzia 1998 hadi 2002. Alichagua kuwa mwenyekiti wa Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA) mwaka 2002.


Adam shafi ameandika vitabu vyengine zaidi ya vitatu, vikiwa ni riwaya: Kasri ya mwinyi Fuad – ambacho kimetafsiriwa kwa Kifaransa, Kirusi, na Kijerumani; Kuli, Vuta n’kuvute na Haini.


Mafunzo Kitabuni.


  • Mungu hamyimi mja wake riziki.

  • Si  haki hata kidogo kumhukumu mtu kwa nasifu wa sura yake, hasa pale mtu huyo anapokuomba msaada kwa shida aliyomkabili.

  • Ukipata itumie ukikosa ililie.

  • Endelea na safari tu bila kujali shida na mashaka yaliyo mbele yako.

  • Penye nia pana njia.

  • Kwenye nchi ya vipofu chongo ni mfalme.

  • Mungu siku zote anakuwa pamoja na wale wenye kutawakali.

  • Kwa yeyote uliyokuwa na roho ya utu; mambo ya kishenzi, huwa yanaudhi kuyaona.

  • Hofu mnapokuwa wengi ina afadhali katika hofu unapokuwa pweke.

  • Ndoto humpaisha mtu kutoka dunia ya kweli hadi akhera!

  • Aumwae na nyoka akiona ung’ongo huogopa.

  • Penye waliovaa midabwada hata ukivaa nguo za viraka utaonekana mtanashati aliyependeza.

  • Kimya kingi kina mshindo.

  • Kusema ukweli ni thawabu kwa wote ndani ya wanaoamini.

  • Siku zote kuna mwanga mwisho wa pango.

  • Msafiri ni aliye pwani.

  • Shukuru kwa kile ulichopewa.

  • Pokea hidaya ingawa dhaifu.

  • Baada ya dhiki faraja.

  • Safari ni hatua.

  • Ngoma ya kitoto haikeshi hata usiku mmoja.

Utamu wa Kiswahili


“Ndoto zetu ziliyoyeyuka, matumaini yetu yalivurugukika. Tulikataa tamaa, tulivunjika moyo.”

“... sikuvunjika moyo kiasi cha kukata tamaa”

“...imani thabiti ndani ya moyo wangu kwamba binadamu asingeliweza kushindwa na namna ya kuishi mahali popote”


‘ … Dhiki yote ile iliyokuwa imenizonga niliona kuwa ni mashaka ya muda tu yanakuja na kuondoka katika maisha ya binadamu.”


“ … nilitamani nipate upenu ulio mahali penye utulivu na kivuli kizuri, nikae hapo kwa kupumzika.’


“Watu wanasema duniani sura ni mbilimbili. Hutokea watu wasiohusiana hata kidogo wakafanana.”


“ yaliendelea kule majahwa yalipokelewa, maisha ya kuishi kwa buruma, imani na takrima za watu wengine”


“ nilifurahi moyo wangu ulichanua kama ua liliopata umande wa alfajiri.”


“Mawingu yalikuwa yamekoza rangi ya manjano, ndimi za jua zilianza kutoa ishara za kwamba jua, mfalme wa mchana, tayari likitaka kuchukua utukufu wake”


“… kule wanakoishi mahambe, wasiokuwa na chochote, hali zao hohe hae.”


“ tulipofika kwake tulipokewa na mke wake. Bibi siti, aliyekuwa mpole, mwingi wa huruma na aliyetupenda kama watoto aliowazaa wenyewe.”


“... wote kwa pamoja walipiga mayowe kuomba tahafifu kutoka kwa askari wale waliokosa utu na insafu.”


“... alitukabili kwa mlahaka wa uso uligua ukunjufu na sisi tuliona afadhali , tumepata mtu wa kuzungumza naye.”


“ nilikuwa mbali na kwetu, nilikuwa mbali na kila aliye wangu. Sina baba, sina mama, sina ndugu, sina jamaa. Nilikuwa mimi na Mungu wangu tu.”


“… niliamini kwamba siku moja nitafika tu. ‘ Penye nia pana njia”. Lakini njia yenyewe ilikuwa imejaa visiki na vichuguu. Kila nilipopita vilinikwaa na kuniangusha. Njia yenyewe ilikuwa haipitiki kwa urahisi na aliyetaka kuipita ilimlazimu awe na moyo.”


“ … hayo mimi niliyazoea na moyo wangu ulikufa ganzi. Nilichoshindwa kukizoea ni ile hofu iliyokuwa ikimjia kila tulipolivuka daraja la Nzozia, hasa wakati ambao mapenzi humvaa Kassim ukadhani yamemtia wazimu.”


“... wasiomjua waliodhani mwendo ule wa kasi wa basi la kwiva ulikuwa ni sababu ya ubingwa wa dereva wake. Sisi tuliomjua tulielewa vyema siri ya haraka zake.”


“Alinisogelea karibu, “ Twende zetu”, aliniambia… “wapi?” nilimuuliza… “ popote pale ambapo tutakuwa mimi na wewe tu. peke yetu, pale ambapo walimwengu wengine hawataweza kufika” aliniambia.”


“ yeye ni mwenzangu tuliyekuwa naye pamoja na mchezo  wetu wa utotoni ulikuwa mmoja kumwona pale Bugoma ilikuwa ni sawa na kuuona mti mzuri umestawi katikati ya jangwa.


“ … Haikuwa njia ya kistaarabu ya kuondoka, hasa mahali ambapo mtu alipokelewa vizuri, akaenziwa akajenga usuhuba na kila mtu. Lakini sikuwa na jingine la kufanya. Ilinibidi niondoke hivyo.”


“... King’ora kilipolia kuashiria kuondoka kwa treni; nayo wangu ulichanua kama linavyochanua wa lililonyonyotewa na uwanda wa alfajiri.”  


“... Mzungu alinibadilika ghafla, uso uliomsanjika ulikuwa umeiva kama balungi.”


“…  nilikuwa nimesimama mbele yake uchi. Sikuwahi kupatwa  na idhilali kama ile. Yakukashifiwa, kudhalilishwa na kushushiwa hadhi ya utu wangu.”


“ Walikuwa wakiishi wakati wa Adam na Hawa, kabla Adam hakulila tunda alilokatazwa na Mungu asilile katika bustani ya Eden. wakati uchi ulipokuwa si kitu cha kusitiriwa wala kuonewa haya.”


“ Harufu nzuri ya mikate waliyokuwa wakichoma haikufaa chochote mbele ya harufu ya kukirihisha ya najisi aliyokuwa akitoa yule mtoto.”


“ usiku ulipita kwa haraka kuona kama uliopeperushwa kwa upepo. Mara mawio yalianza kuingia.”


“ Tabu, dhiki na mashaka yetu nilikwishayazoea. Kwahiyo kulalia maboksi na tofali kuwa ndiyo mto wangu wa kuwekea kichwa halikuwa jambo la kuniletea tafara na kuninyang’anya raha ya usingizi wa usiku.”


“... haikuwa rahisi kwa wageni kama sisi kujitoma tu mahali kama pale bila ya kukaribishwa au kualikwa. Huo ungelikuwa ni udoezi; na kudoea si jambo la insafu hata tungelikuwa na njaa kiasi gani”


“ Mbele ya mpwango, mswahili huna la kumwambia. Kwa hivyo nilijaza sahani yangu wali tele.”


“… Tulipata utulivu wa roho na akili na wasaa wa kufikiri juu ya safari yetu iliyokuwa imejaa kisirani na ukorofi.”


“... sikuweza kurudi kule nilikotoka sifiki kule nilikotaka. Nilikuwa nimo tu nikipigwa na mawimbi ya tabu na mashaka ya maisha. Nilitamanii kujuta lakini kujuta ingelikuwa ni kukubali kushindwa. Mimi sikutaka kukubali kushindwa.”


“... Mavazi niliyovaa mimi hayakuwa ya mtu mtanashati lakini penye waliovaa midabwada hata ukivaa nguo za viraka utaonekana mtanashati aliyependeza.”


“... kama nia yangu ya kukawia kurudi nyumbani usiku ule ilikuwa ni kujua usiku wa Khartoum ulikuwa na nani? Watu au afiriti na maluuni, basi niliyekuwa naye usiku ule ulikuwa afiriti, tena afiriti aliyejua umaluuni.”


“... siku mpya ilianza kama ziliyoanza siku nyengine zote zilizopita. Kwa kujawa na subira na kuwa na matumaini, labda leo. Kila siku mpya ilikuwa hivyo labda leo… labda leo, lakini leo nyingi. Zilizopita na leo ya siku ile tulikuwa na matumaini pia.


“ Lakini tungelifanya nini? Ilikuwa lazima tusubiri. Tusubiri na kusubiri kwani mustakibali wetu ulikwepo kutoka kusubiri  kwani mustakibali wetu ulikwepo katika kusubiri. Tumeambiwa kuwa “ subira ya vuta kheri”.”


“... kichwani mwangu nilikuwa na mgongano wa mawazo yale yaliyosema mstamilivu hula mbivu yakivutia upande mmoja. Yale yaliyosema mstamilivu hula mbovu yakivutia upande mmoja.”


“... kwanza alitaka kujua hali yetu. Nilimjibu kuwa hali yetu kama yake, sisi tulikuwa wazima na tunamshukuru Mwanga kwa hili.”

“ Kwakuwa usiku na wakati ambao usingizi humpumbaza. Binadamu ukamfanya asiwe na lolote aliwezalo ila kulala tu, kila mtu alikuwa amelala au akisinzia.


“... siasa ilikuwa imestawi. Siyo kama yanayostawi maua ambayo humfurahisha kila aliyetazama bali kama unavyostawi upupu ambao humuwasha kila aliyegeuka.


“ Ala! Kumbe nyoka na ujeuri wake wote, huwa chuchu anapokutana na cheche!”


“... nilitaka kuliokota ili kumpiga nyoka yule. Lakini nilijiuliza, karara lingelimfanya nini nyoka yule? Nyoka alitaka fimbo, fimbo ilikuwa mbali na pale nilipokuwepo; na fimbo ya mbali haiui nyoka!”


“ ‘Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu’ mimi nilifunzwa na wote. Nimefunzwa na mama yangu aliyenifunza kukinai, kuvumulia, na kustahamili na nimefunzwa na ulimwengu ulionifunza tabu; shida na mashaka.”


“ Moyo wangu ulichanua kama ua lilpnyonyotewa  na umande wa alfajiti”


“ …Jahili nisiyejua nililotaka kulifanya…”





 


 


 










You Might Also Like

0 #type=(blogger)

Top Categories