Tumbo Lisiloshiba

 

Tumbo Lisiloshiba na Hadithi nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupinzilizoandikwa na waandishi waliobobea na wale wanaochipuka katika uandishi wa utanzu wa hadithi fupi. Hadithi katika mkusanyo huu zimeandikwa kwa ubunifu na kwa kuzingatia maswala ibuka katika jamii inayokwenda ba utandawazi na usasaleo.

Utangulizi


Tumbo Lisiloshiba na Hadithi nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupinzilizoandikwa na waandishi waliobobea na wale wanaochipuka katika uandishi wa utanzu wa hadithi fupi. Hadithi katika mkusanyo huu zimeandikwa kwa ubunifu na kwa kuzingatia maswala ibuka katika jamii inayokwenda ba utandawazi na usasaleo.


Mkusanyo huu unaangazia maudhui mbalimbali kama vile: Siasa, dini, ulemavu, masuala ya kijinsia, elimu, ukware, ulaghai, uchumi, mazingira, umaskini, uongozi, ukabila, mapenzi, ndoa, ushirikina miongoni mwa mengine. Masuala yaliyoshughulikiwa katika mkusanyo huu yataibua ilhamu ya msomaji, msomi, mtafiti na wanafunzi katika maisha yao.


Maudhui, mtindo, lugha na uhusika ni viungo vilivyosukwa kwa namna ya kipekee katika mkusanyo huu.


Tumbo Lisiloshiba na Hadithi nyingine; imekusanya hadithi kumi na tatu; Tumbo lisiloshiba, ‘ Mapenzi ya Kifaurongo’, Shogake Dada ana Ndevu, Shibe inatumaliza, mame bakari, masharti ya kisasa, ndoto ya mashaka, kidege, nizikeni papa hapa, tulipokutana tena, mwalimu mstaafu, mtihani wa maisha na mkubwa.


Waandishi


 Said A. Mohamed; ni mwandishi maarufu wa kiswahili aliyezaliwa Unguja. Kwa sasa ni Profesa wa Fasihi na Lugha za Kiafrika. Amefundisha Fashi ya Kiswahili katika vyuo vingi kote duniani. Ameandika vitabu vingi katika mawanda yote ya Fasihi Andishi.


 Kenna Wasike; ni mzawa wa Kenya na ni miongoni wa waandishi chipukizi wanaoonyesha matumaini makubwa katika uandishi wa kazi za kubuni za Kiswahili. Kenna ana shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.


Alifa Chokochoko; ni mwandishi chipukizi mwenye uwezo usiokadirika wa kubuni hadithi. Yeye amekuwa mwalimu wa somo la Fasihi kwa muda mrefu katika shule mbalimbali. Bw. Alifa ameandika makala mbalimbali ya Kiswahili.


Salma Omar Hamad – ni mhadiri msaidizi katika chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Ni msomi na mtaalamu maarufu katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Ana shahada ya uzamili katika Isimu, lugha ya kiswahili. Kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kwa sasa anaendelea na shahada yake ya Uzamifu katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Ameandika kazi kadhaa za ubunifu za fasihi.


Mohammed Khelef Ghassany ni mzawa wa Zanzibar ambaye ni mshairi na mwandishi wa hadithi fupi. Kwa sasa ni mwanahabari katika idhaa ya Kiswahili ya Radio Deutsche Welle, ujermani.


Ali Abdallah Ali ni mzawa wa Pemba ambaye ameondokea kuwa mwandishi stadi wa hadithi fupi katika Kiswahili. Amechangia pia mkusanyo wa Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine uliohaririwa na Ken Walibora na Said A. Mohamed. Yeye alisomea shule za msingi na upili huko pemba na kupata mafunzo ya ualimu huko. Unguja kisha diploma ya juu ya kufundisha Kiingereza kule Australia.


Robert Oduori ni mhadhiri mkuu, Chuo Kikuu cha Moi. yeye ni mhadhiri wa Isimu Telekezi na Tafsri katika Idara ya KIswahili. Amefundishwa Chuo cha ualimu, Eregi na shule za upili. Aliwahi kuwa mwalimu wa Kiswahili na Uchumi. Ni mwandishi na mtunzi wa kazi za Fasihi ya Kiswahili zikiwemo hadithi fupi na riwaya. Pia amediriki kazi mbalimbali za tafsiri.


Ken Walibora ni mzawa wa kenya, na mwaandishi maarufu wa Kiswahili. Ni mwaandishi mtajika wa kazi za Fasihi ya kiswahili. Amewahi kuwa mwanahabari wa redio na runinga nchini Kenya. Pia huandika makala ya Fasihi ya Kiswahili katika gazeti la Taifa leo nchini Kenya.


Dumu Kayanda ni mwandishi chipukizi mwenye uwezo wa kubuni hadithi ulio na upeo usiokadirika. Yeye amekuwa mwalimu wa somo la Fasihi kwa muda katika shule mbalimbali. Bw. Kayanda ameandika makala mbalimbali ya Kiswahili.


Eunice Kimaliro ni mzawa wa Kenya, mshairi na mtaalamu wa elimu aliyeandika vitabu kadhaa. Kwa sasa anasomea shahada ya Uzamifu kwenye Chuo Kikuu cha Worcester, Uingereza.


Ali Mwalimu Rashidi ni mwandishi mashuhuri wa Fasihi na mtaalamu wa masuala ya maendeleo ya lugha ya Kiswahili pamoja na sayansi ya jamii. Ameajiriwa na Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni nchini Tanzania kama mkufunzi. Mwaka 1981 – Mei 1985 alijiunga na Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni ambako alitunikiwa cheti na Stashahada ya Lugha na Ualimu. Mwaka 1985 Juni -1988 alijiunga na chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwa masomo ya elimu ya juu na kutunikiwa shahada ya kwanza ya fani ya sanaa na Elimu.


Nukuu kitabuni


  • Fasihi bora ilipasa kuwa bora jana na pia lazima iwe bora leo na kesho.

  • Fasihi bora haipitwi na wakati.

  • Kama mtu amekufa basi amekufa na kama yu hai bila ya shaka yu hai.

  • Ubunaji wa sanaa yeyote ile haulazimishwi.

  • Kuugua sio kufa.

  • Siku hizi wanasheria waaminifu ni adimu kama haki yenyewe.

  • Maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini au tajiri.

  • Polezi katika mambo yenye hatari ni ubaradhuli mtupu.

  • Fasihi inahusu kuielekeza jamii – ni nyenzo mwafaka ya kufanya jamii iwe radhi kuyakabili mabadiliko yaliyoko na yajayo lakini kosa kubwa la wasomaji siku hizi ni kuwachukulia wahusika wa fasihi kama mfano halisi ya kuigwa au kuepukwa; kuiona riwaya kama Biblia au Msahafu.

  • Fasihi kazi yake si sawa na mahaburi ya kanisani ay msikitini. Ni sanaa! Si propaganda. Kubwa zaidi ni kwamba fasihi kila siku inaelekea kuburudisha.

  • Kuuliza sio ujinga bali kuuliza ujinga ndio koasa.

  • Binadamu amepewa uwezo wa kufikiri na kutengeneza mazingira yake yawe mwafaka.

  • Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura, samaki hafunzwi kuogelea itakuaje wewe uliye na utashi ufundishwe kujinadhifisha kesho yako? — Ni ajabu kwamba asichofunzwa mwana wa binadamu ni kula!

  • Mapenzi ni matamu kama uki na ni aula kwa moyo uliovurugika.

  • Ujapokosa la mama hata la mbwa huamwa.

  • Mapenzi kama ule mmea wa kifaurongo. Huwa hai hali ikiwa shwari na shari ikitokea yanajifia na kufufuka hali ikitakata tena.

  • Mzoea vya sahani, vya kigae haviwezi.

  • Moyo wa binadamu ni kama mtoto mchanga, hauishi kujidanganya.

  • Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa hatimaye.

  • Kujipa uhakimu kwa jambo usilolijua si vizuri.

  • Ahadi za mapenzi ni kama kifaurongo, zikiguswa tu zinakufa.

  • Mtu huvuna alipopanda.

  • Mgomba changaraweni haupandwi ukamea.

  • Maneno matamu ya mapenzi ni uongo mtupu.

  • Kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza; ni kama kuota ndoto ukaelekea kiza.

  • Wajinga ndio waliwao – na wakati mwengine hujivika ucha Mungu na kujiliwaza kwa vya aya takatifu inayosema: “ Hadhaa min falhli rabbi – yaani Allah humpa amatakaye bila kiwango maalumu.

  • Tupo kwenye dunia ambayo mataifa wanaangalia watu kwenda kazini na si kufanya kazi.

  • Mafisadi haupakua mishahara na wala si kupokea mshahara – maana kupokea hufuatana na kupewa.

  • Usimchungunze bata utashindwa kumla!

  • Ulimwengu huu hakuna mtu na chake, kila kitu ni cha wote.

  • Kula kuna taratibu zake lakini mwenye njaa hasa hana miko, kanuni wala sheria.

  • Shibe huanza kwenye moyo.

  • Vyovyote iwavyo, tumbo si kigezo cha shibe.

  • Siku zote kinachobaki kwa myonge ni kulia na kuapiza.

  • Dunia ina malipo yake.

  • Hapana gumu lisilogeuzika kuwa laini.

  • Usiku na giza, na giza hufunika balaa zinazofanyika huku unawalinda waovu.

  • Jibu la safii ni sukutu.

  • Wataalamu wa tiba husema kuwa maji yanukiayo waridi hhutuliza moyo.

  • Baada ya dhiki faraja.

  • Kibuyu hakifichi mbegu!

  • Dunia haina siri. 

  • Mapenzi yana uimara wa pekee na msimamo usioterereka. Wengine huyafananisha na majani kuwa hujiotea popote.

  • Siri ya mtungi iulize kata au kitanda usichokikalia huwajui kunguniwe!

  • Apewaye ndiye aongezwaye.

  • Aliye maskini kabisa hapendi.

  • Subira ni ufunguo wa kheri.

  • Kila chenye mwanzo na mwisho kinao.

  • Mambo madogo huzalisha mambo makubwa.

  • Mwacha kiwi hanacho na chema kimpotelee 

  • Watu wa majiji makubwa kuona ajabu kwa mambo ambayo hata wao huwakuta kila siku.

  • Ni rahisi kusema utaandika kuliko kuandika hasa; mjenzi hasemi nitajenga, hujenga tu.

  • Mdharau biu hubiuka.

  • Mali bila daftari hupotea bila ya habari.

  • Waliosema masomo si biashara wanaishi sayari nyengine.

  • Shule si sababu wala udhuru wa kufanikiwa au kutafanikiwa maishani.

  • Huwezi kushindwa na mtihani wa shule na vilevile kushindwa na mtihani wa maisha. Mungu hamkoseshi mja wake yote.

  • Mwana hutazama kisogo cha nina.

  • Kuku mgeni usimtoe nje.

  • Huwezi kukataa dau wakati pa kuvuka pana habari.

  • Ajali haina miadi.

  • Usilipe jema kwa baya.

Ujumi Kitabuni na Utamu wa Kiswahili


“ tena nikwambie kuwa mambo mengi mazito husaulika haraka. Kama si mambo mazito basi mabadiliko muhimu yangepiga kasi harakaharaka. Uzuri lakini sisi tumeumbwa na sahau, ingawa sahau hiyo ni tokea lilelile la ‘umoja’ katika ‘uwili’. Upande huu wa sahau hutupa ‘nafuu’ na upande ule ‘balaa’, ingawa nafuu ndiyo tunayochelewa kuisahau na balaa ndiyo inayodumu kwa muda mrefu ndani ya kumbukumbu zetu.


“ Mola ndiyo atowae akampa mahaluki

Humpa amtakae huyo ndo humbariki

Na kila amnyimae kupata hatodiriki.

Mpewa hapokonyeki, aliyepewa kapewa.

Hata ukifanya chuki, bure wajisumbua.”


“ Dunia we’dunia. Dunia ya mwenye nguvu, si ya mimi dhaifu wa nguvu. Dunia ya msumari moto juu ya donda bichi. Hao watu nao je?”


“ Mbali ya kuwa wazo hilo kwake ni kubeba dhamana nyengine. Zaidi aliliona ni njia ya mkato isiyo na busara yeyote. Kamani kufa, si yeye aliyestahili kufa. Yeye ni mkosewa si makosa. Ni mdeni si mdaiwa, yule dhalimu mkuu wa mdhalimu.”


“ Ahadi ya kale ni ileile, Sara, alikumbusha Sarina: ‘chako ni changu, changu ni chako. Mmoja akianguka, mwenziwe amwinue. Mmoja akiacha, mwenziwe aendeleze.’ kiapo kikawa kimetimia na mzigo ukawa umepata wachukuzi.


“ Lakini sara alikuwa hayu hai hayu maiti, yupo katikati alikuwa anavaa wala haoni, anasikia wala hasikii, anahisi wala hahisi, kwake ile ilikuwa nusu ndoto na nusu kweli.


“... Wanafunzi wote hao wanafunzi wake hawamsahau kwa nasaha zake, kwa insafu yake, kwa huruma zake, kwa hekima yake, kwa ustaarabu wake, kwa udalifu wake, kwa uwajibikaji wake, kwa neusi yake, kwa ucheshi wake, kwa ukaramashi wake – kwa yote na yote.


You Might Also Like

0 #type=(blogger)

Top Categories