" Usirithi Adui wa Mtu" - Dkt. Jakaya Kikwete.


Photo credit: UDSM Gallery


 



Hii ni sehemu ya hotuba aliyotoa Rais mstaafu wa awamu ya nne katika Chuo kikuu cha Dar es salaam, 11 Disemba, 2017.


Nakala


Profesa Lingise, niseme kwa kiswahili.


Aah! Nilisema siku moja kwenye mkutano fulani mmoja hivi lakini…


Nilipo hamishwa kutoka Monduli na kupelekwa Nachingwea, mkuu wa wilaya wa pale… Nilipelekwa  kuwa katibu wa wilaya, nimetoka kwenye jeshi nikapelekwa kuwa katibu wa wilaya.


Mkuu wa wilaya pale, kwenye mkutano, hafla ya kunikaribisha akaniambia “ eeh bwana sikiliza, umekuja hapa mgeni, kuna watu watakuja kuambia hapa bwana ili ufanikiwe, haki ya Mungu; kama fulani yupo, mambo yako  yatakuwa yameharibika. Na wanaofaa hapa nakuambia ni fulani… fulani; hawa ndio watakao kusaidia”


“Ushauri wangu kwako; usirithi adui wa mtu, tengeneza adui wako. Na  ushauri wangu kwako hakuna haja  sababu ya kutengeneza adui. Ni jambo halina tija. Mchukulie kila mtu vile alivyo, sio kwa kuambiwa. Utakapo Fanya kazi utajua nani ni nani?


Ndiomana akili za kuambiwa  changanya na za kwako.


That was my advice from my neighbour's brother, from your Chancellor.


Good luck!  


 .



You Might Also Like

0 #type=(blogger)

Top Categories